Follow By Email

Tuesday, 25 November 2014

Ndugai amenguliwa mjadala wa Escrow?


Safari ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai (Pichani), nje ya nchi imehusishwa na mpango wa kudhibiti mjadala bungeni unaohusu uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Habari za Ndugai kusafiri zilianza kuenea Alhamisi wiki iliyopita, huku zikidai kwamba, ni mikakati iliyopangwa dhidi yake kutokana na hatua yake ya kutaka ushauri kwa wabunge kuhusu nini kifanyike kuzuia mihimili mingine kuingilia utendaji wa Bunge.

 Ndugai alitoa fursa hiyo baada ya wabunge kuomba mfululizo miongozo ya Spika bungeni, kuhusiana na kashfa hiyo.

Wabunge walifikia hatua hiyo baada ya awali kuibuka madai na baadaye Bunge kukana kuhusu kuwapo kwa barua iliyoandikwa na Mahakama ya Tanzania, ikidaiwa kuzuia suala la Escrow kujadiliwa bungeni, kwa madai kwamba, lipo mahakamani.

Katika kuhitimisha ushauri aliopewa na wabunge wasiopungua saba, Ndugai aliahidi kutumia kanuni na sheria za Bunge ipasavyo na kusema atarejea misimamo ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samwel Sitta, kukataa umoja wa kulinda maovu.

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa baada ya jitihada za kumtaka Ndugai kusikiliza maelekezo kugonga mwamba, ndipo ikaamriwa asafiri kwenda nchini Uingereza kwa muda usiopungua siku 10.

Chanzo kinasema kuwa Ndugai amewekwa pembeni ili asisimie mjadala wa sakata hilo bungeni.

Taarifa zaidi zimedai kuwa Ndugai ameambiwa kuwa amepewa kazi maalum nje ya nchi ambayo ataifanya kwa siku 10 na atakaporejea atakuta mjadala wa Escrow bungeni umemalizika.

“Msimamo wake wa kusimamia suala hilo ili lijadiliwe bungeni na kutoa nafasi kwa wabunge wiki iliyopita kutoa ushauri kwa kiti cha Spika ndilo lililomponza,” kilieleza chanzo kimoja.

Vikao vya Bunge siku ya jana, viliendeshwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye kwa muda mrefu tangu Bunge lianze hakuwapo na inaelezwa kuwa ndiye tegemeo la wanaotaka mjadala huo udhibitiwe.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, aliliambia NIPASHE jana kuwa, ingawa ni kweli Ndugai anasafiri, habari zinazohusisha safari yake na suala la Escrow bungeni ni za uzushi.

“Ni kweli Naibu anasafiri nje ya nchi, lakini kwamba ni kutokana na masuala ya uendeshaji wa vikao ni uzushi tu jamani, tena anaondoka kesho. Hebu mpigie yeye ndiye atawaeleza kwa uwazi kinachoendelea,” alisema Joel.

KAULI YA NDUGAI
Ndugai alipoulizwa na NIPASHE jana kuhusiana na taarifa hizo, hakupatikana. Hata hivyo, juzi jioni alipoulizwa, hakutaka kulizungumzia suala hilo zaidi ya kujibu kwa ufupi kupitia simu ya kiganjani:“Naomba jambo hili tuliache kama lilivyo.”

WABUNGE WANASEMAJE?
Baadhi ya wabunge waliozungumza na NIPASHE jana kuhusu fununu zinazohusu safari ya Ndugai namna anavyoongoza vikao vyao wakilinganisha na uongozi wa Makinda.

Kangi Lugola (Mwibara-CCM) alisema vikao vyote vya Bunge hutakiwa kuongozwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizoidhinishwabna kwamba, tatizo siyo Ndugai wala Makinda, bali ni wabunge wenyewe kuwa wanafiki.

“Kila mmoja lazima awe na tofauti na mwingine katika kutumia kanuni, kwa kuwa kila mmoja ana uwezo tofauti na mwingine katika kutumia na kutafsiri kanuni, hivyo ni jukumu la wanaoona tofauti kusema kwa wazi kuwa hakutendewa inavyotakiwa,” alieleza Lugora 

Alisema Spika siyo mwenye mamlaka ya mwisho ya Bunge, bali wabunge wenyewe na kutaka wabunge watakaoona spika anapeleka Bunge ndivyo sivyo, wasimame bungeni na kuchukua hatua sitahiki siyo kulalamika pembeni.

Aliwataka kuiga kwake alipowasilisha hoja kuhusu kashfa ya oparesheni tokomeza kwamba alimudu kuzuia mipango ya kuipindisha mpaka haki ikatendeka.

Haroub Muhammed Shamis (Chonga-CUF) alisema kuna tofauti kubwa kati ya uendeshaji wa vikao kati ya Ndugai na Makinda, hali anayoihusisha na umri wao.na kuendelea kuongoza tofauti na mama ambaye anakaribia kustaafu,” alisema Shamis.

Tundu Lissu (Singida Mashariki-Chadema) alisema ingawa hafahamu lolote kuhusu safari ya Ndugai, suala la uendeshaji wa vikao vya Bunge lipo wazi na linafahamika na wabunge karibu wote.

“Kwenye masuala nyeti na ya msingi kama la Escrow, tabia ya Spika ni kuzima mjadala, wakati kwenye mambo ya msingi tabia ya Ndugai, ni kuruhusu mjadala, wako tofauti kabisa,” alisema Lissu.

MBINU CHAFU
Wakati hayo yakijiri, vitabu vyenye picha na magazeti yanayoeleza habari binafsi na kumshambulia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, vilikuwa vikisambazwa na kugaiwa bure kwa wabunge bungeni.

Kusambazwa kwa vitabu hivyo na magazeti kunahusishwa na njama za kutaka kukwamisha mjadala bungeni kesho kuhusiana na ripoti ya uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika akaunti ya Escrow.

NIPASHE  iliwashuhudia wabunge wakiwa na vitabu hivyo,  wakiwa wanasoma kwa kupokezana.Walioshuhudiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mbali na hao pia wabunge kadhaa walionekana wakiwa wameshika nakala ya kitabu hicho kilichosomeka ‘Mjue Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mtetezi wa Watanzania wanyonge’.

Katika kitabu hicho ambacho NIPASHE imefanikiwa kukiona na kukisoma, zimewekwa tuhuma kadhaa na masuala binafsi ya Zitto yanayoeleza namna anavyoshiriki wizi kwa kutumia watu katika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya wabunge wa CCM na upinzani waliponda hatua hiyo na kusema ina lengo la kutaka kuzima mjadala wa uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Escrow.

Mbali na hilo, pia zilikuwa zikisambazwa nakala za gazeti moja la kila wiki (jina tunalo), ambalo lilikuwa na toleo maalumu, lililokuwa likigawiwa bure kwa wabunge na wageni mbalimbali.

Katika gazeti hilo, ambalo lilikuwa na kichwa cha habari kilichosomeka ‘Sakata la IPTL Zitto kuliingiza Bunge kwenye mtego wa hatari’.Gazeti hilo, ambalo Mwenyekiti wake wa bodi, Prince Bagenda, lina picha ya Zitto na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Lilikuwa likigawiwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Epson Kadya, ambaye ni meneja masoko na usambazaji wa gazeti hilo, ambaye alisema lengo la kugawa bure ni kutaka watu wajue ukweli kuhusu sakata hilo

WEREMA ATAHADHARISHA
Siku mbili kabla mjadala huo kutinga bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, amelitahadharisha Bunge kuwa makini katika kulijadili sakata la Escrow.

Akizungumza jana jioni bungeni wakati wa kufunga mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2014, alisema kwamba kwa sasa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inafanya uchunguzi wa kimahakama, hivyo unatakiwa umakini.

“Nawaomba msichafuane katika mitandao, watu wameanza kulalamika kuhukumiwa kabla ya kusikilizwa,” alisema.

NA MUHIBU SAID
CHANZO: NIPASHE

Mkono asimulia alivyonusurika kifo London


Dar es Salaam. Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ambaye hivi karibuni alinusurika kifo akidaiwa kulishwa sumu akiwa London, Uingereza amesimulia jinsi tukio hilo lilivyomkuta.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkono alisema endapo uchunguzi wa suala hilo utakamilika na kuthibitisha kwamba alilishwa sumu, atapambana na wahusika kwa kuwa wamehatarisha maisha yake.

Mkono ambaye pia ni wakili maarufu nchini, alitoa kauli hizo jijini hapa jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mwenendo wa afya yake.

Alidai kwamba, lengo la kumlisha sumu ni kuharibu figo zake ndani ya saa 72 wakati alipokuwa katika ziara ya nchini humo.

“Niko vizuri na afya njema… kama kuna mtu anawinda jimbo langu mwambieni ameshindwa na wananchi wangu nawaeleza kuwa niko salama wasiwe na hofu. Ninataka kujua nani kanilisha sumu na kwa nini?” alisema Mkono.

Akisimulia tukio hilo alisema, Novemba 11 akiwa miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, walisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Uingereza akiwa salama salimini.

Aliwataja baadhi ya wabunge walioambatana nao kuwa ni William Ngeleja (Mwenyekiti wa kamati hiyo), Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika.

“Tukiwa uwanja wa ndege nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi (hakutaka kuuweka wazi kwa sababu upelelezi haujakamilika), ukinitahadharisha kuwa makini, ujumbe ule ulinishtua kwa kweli.”

“Niliwaonyesha wenzangu niliokuwa nao na pale tulikunywa chai kabla ya kuondoka na tulipofika kule mimi nilikaa hoteli yangu na wenzangu wakakaa ya kwao,” alisema.

Huku akisimama na kunyoosha mikono kuonyesha yuko vizuri, Mkono alisema siku iliyofuata ratiba iliwataka kuhudhuria Bunge la Uingereza.

“Niliamka na kwenda Ubalozi wetu na kwa kuwa tulitakiwa kufika bungeni saa 5.00 asubuhi, niliwahi na wenzangu na walipokuja tuliungana… tulipokuwa ndani katika Bunge la Uingereza, ghafla nilianza kujisikia vibaya hali iliyonisababisha nipoteze fahamu kwa saa sita. “Lakini kabla ya kupoteza fahamu niliwaeleza wanipeleke nyumbani (Tanzania), wenzangu wanasema nilikuwa napiga kelele, nirudisheni hawa wanataka kuniua,” alisema Mkono kwa sauti ya chini na kuongeza:

“Hapa nasimuliwa sasa kuwa walinipeleka hospitalini na waliponifikisha madaktari wa pale waliamua kuwasiliana kwanza na Daktari wangu, (Lusangulila Kapitain) ili kujua kama wakati natoka Tanzania nilikuwa na tatizo.”

Alisema, “Kapitain baada ya kuelezwa hali niliyonayo naye aliwaeleza kuwa huyo (Mkono) atakuwa amelishwa sumu kwani wakati anatoka huku alikuwa salama kabisa na akawaomba wanipatie dawa ambazo zilinirejesha katika hali yangu ya kawaida kuanzia saa 12 hadi saa moja jioni.”

Mkono alisema kitu ambacho hadi sasa hajakielewa na anapenda kukifahamu ni kwa nini na malengo yapi akisema kama ni sakata la escrow lilikuwa wazi bila kificho.

“Serikali ilikuwa ni mteja wangu katika kesi kati ya Tanesco na IPTL… nikiwa bungeni siwezi kuongea hadi nipate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutokana na maadili ya kazi zetu, lakini uchunguzi ukibainika kwamba nililishwa sumu kwa sababu hiyo nitaweka kando maadili ya kazi.”

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

What is a Jewish nation state?

Palestinians pray in front of Dome of the Rock in the Al-Aqsa Mosque compound [Getty Images]

The Israeli government is dropping the pretense of balancing the state's Jewish and democratic nature.

The "Jewish nation-state" law, already approved by the Israeli cabinet on Sunday and yet to be presented for a vote in the Knesset this Wednesday, will enshrine in statute a situation that has been palpable on the ground for decades. Its discriminatory character, turning a large Arab Israeli minority into second-class citizens and delisting Arabic as an official language, will only confirm the ongoing discrimination that members of this group have been subjected to well before the drafting of the new law.

The fallout from this piece of legislation is likely to be purely symbolic, marking a shift in the Israeli ideology hailed by some right-wing elements of the Netanyahu government as a return to the basics of Zionism.

The schizophrenic self-presentation of the State of Israel as Jewish and democratic is coming to an end in a clear choice of the polity's Jewish and non-democratic fibre. But exactly what does a "Jewish nation-state" mean?

The ideologues of the regime are quick to point out that there is no inherent tension between France being a French and democratic state, or Germany being a German and democratic country. But neither Frenchness nor Germanness is equivalent to Jewishness. Even if the majority of citizens in France and Germany are Christian, these states are not declared to be "Christian nation-states".

Definition of Jewishness

So what if Jewishness were not identical to Judaism, that is to say, to the Jewish religion? In fact, the official discourse in Israel has been, for a long time and purposefully, blurring the distinctions between religion, nationality, and ethnicity.

The very definition of Jewishness according to the 1950 Law of Return is ambiguous, seeing that the two possible criteria are: having a Jewish mother or converting to Judaism. The first criterion is biological, while the second is religious.

Amendment 2, passed in 1970, accentuates the religious component, bestowing the right of immigration on "a child and a grandchild of a Jew, the spouse of a Jew, the spouse of a child of a Jew and the spouse of a grandchild of a Jew, except for a person who has been a Jew and has voluntarily changed his religion". In other words, it is not enough to have been born of a Jewish woman in order to be considered a Jew; the act of conversion from Judaism to another faith would be grounds for excluding the convert from this definition. One wonders what happens under the Law of Return to the self-professed atheists born of Jewish mothers.

It is apparent that non-Jewish citizens of a Jewish state will find themselves in a limbo, regardless of the vacuous guarantees of "equal personal rights" under the law awaiting approval. But, as I have mentioned above, their predicament has been dire well before the drafting of this bill. The question, then, is why is the Israeli government dropping the pretence of its ability to balance the state's Jewish and democratic nature now, at this precise moment?

Beyond the politicking considerations of a coalition dominated by right-wing hardliners, there are at least two possible explanations for the timing of the proposed piece of legislation.

Major stumbling blocks

First, it attempts to codify a narrative that equates the land occupied by the State of Israel with the "historic homeland of the Jewish people". With these words enshrined in the law, yet another obstacle will arise on the path to peace with the Palestinian people, who will be not only materially and symbolically, but also legally dispossessed of their land and their history.

The words I have cited from the draft legislation usurp the historic origin as the exclusive property of one group of citizens and turn a deaf ear to the rightful claims of another group. Moreover, they render the Jewish attachment to a distant past more important than the ongoing presence of non-Jewish inhabitants in the same territory. All these are major stumbling blocks in the peace process, which will be guaranteed to stay fruitless if future Israeli governments are bound by the "Jewish nation-state" law. For instance, in accordance with it, the right of return for Palestinian refugees will be outright denied on the grounds that the territory claimed by Israel was not their historic homeland.

Second, and more cynically: Could it be that the current rulers of Israel have made a calculated, conscious choice to weaken their emphasis on democracy? Although, in order to gain admission into the international community, it is still necessary to present one's state as democratic, the time of this requirement's non-negotiability might be coming to an end.

Widespread passive acceptance of technocracy and the dictates of the "Troika" in the European Union are the telltale signs of a gradual departure from democratic rhetoric and political practice. It would not be surprising that the Israeli right-wing politicians are ahead of the curve in an avowed abandonment of democratic discourse, and that the draft bill is but a symptom of this lamentable development.

Michael MarderMichael Marder is IKERBASQUE Research Professor at the University of the Basque Country, Vitoria-Gasteiz, Spain. His most recent books include Deconstructing Zionism: A Critique of Political Metaphysics (co-edited with Gianni Vattimo), The Philosopher's Plant: An Intellectual Herbarium, and Pyropolitics: When the World Is Ablaze.

 Al-Jazeera

Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni


Nianze kwa kukuuliza wewe mzazi; unapoweka picha ya mtoto wako kila hatua tangu akiwa mchanga hadi anaanza kutembea na kuanza shule, alikuomba au ulipata ruhusa yake?

Ingekuwa wewe umepigwa picha bila idhini yako halafu ukaikuta kwenye mtandao utafurahi?

Najua unampenda mtoto wako na ana haki zake za msingi pamoja na kuheshimiwa faragha yake popote alipo. Haiwezekani chochote anachofanya ukiweke kwenye mtandao.

Naomba kueleza madhara yanayoweza kutokea kwa kuweka picha za mtoto wako au wa mwenzako kwenye mitandao hasa mitandao ya kijamii kama facebook , instagram na mingineyo.

Kwanza fahamu kuwa kampuni karibu zote za mitandao ya kijamii zimesajiliwa Marekani, chache zimesajiliwa Ulaya na Asia, lakini karibu zote zinatumia sheria na sera za mataifa hayo.

Katika mataifa hayo wanasisitiza mtoto asijiunge kwenye mitandao ya kijamii hadi atakapofikisha miaka 13, wengine miaka 15 au 16 .

Kampuni zote za mawasiliano zina utaratibu wa kuhifadhi kila kitu kinachotokea kwenye shughuli zao za kila siku kwenye chombo maalumu cha kuhifadhi taarifa za mtandao (server). Kwa hiyo ukiweka picha za mtoto zinahifadhiwa huko hata kama utazifuta.

Hapo awali, nilisema mtoto anahitaji faragha yake, unaporusha picha za mtoto wako kwenye hii mitandao au mawasiliano yoyote, unaingilia faragha yake na huko mbele anaweza kukushtaki wewe au wengine walioingilia faragha yake.

Mtoto anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano .

Umeshawahi kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu kwenye mitandao hasa ya kijamii ? unajua ni kwa nini ?

Kwa sababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na ndugu zake.

Kama ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na ‘mabazazi’ kwa sababu ya picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja akabakwa.

Siku hizi kuna biashara ya kutangaza ngono mitandaoni ukiweka picha ya mtoto hujui kina nani wanaangalia na kwa matumizi gani. Wapo wanaoweza kuitumia picha hiyo kutangaza kuwa mwenye picha anafanya biashara ya ngono, utajisikiaje kama mzazi?

Hata hivyo, picha ya mtoto wako inaweza kutumika kutangaza biashara fulani bila wewe kujua. Haya yameshatokea.

Kwa kuweka picha ya mtoto wako, unatoa fursa ya kunyanyaswa na kufanyiwa vituko vingine mbalimbali shuleni au popote atakapokwenda au kwenye kurasa zake mwenyewe za facebook.

Pia siku hizi kuna mitandao na tovuti nyingi zinazotengenezwa kila siku, mtu anaweza kutumia picha ya mtoto wako kutangaza tovuti yake, blogu au bidhaa zake mbalimbali bila ruhusa yako wala ya mtoto wako.

Jijini Dar es Salaam kuliwahi kutokea mzazi kufiwa na mtoto wake maeneo ya Kimara, aliposambaza picha akaweka ya mfano, kumbe picha hiyo ni ya mtu mwingine, watu kwenye mtandao wakajua ndio mtoto halisi.

Sikutishi ila nasisitiza mzazi uheshimu faragha ya mtoto wako na taarifa zake nyingine zinazomuhusu.

Na Yona Fares, Mwananchi

Jeshi la Nigeria huwakimbia Boko Haram


Bodi hiyo inayoongozwa na Sultan wa Sokoto,imesema kwamba jeshi hilo limekuwa na tabia ya kutelekeza silaha zao kwa jeshi na kukimbialia mafichoni , na pindi mambo yanapotulia hurejea uraiani na kuwatishia raia.

Maelfu ya raia wa Nigeria wamekimbilia Niger kufuatia shambulio la hivi karibuni kutoka kwa kundi hilo la Boko Haram.

Waasi hao hujifanya kuwa ni wafanyabiashara walobebelea maboksi yenye bidhaa sokoni katika mji wa Damasak mji ulio Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Lakini imebainika kwamba boksi hizo huwa zimesheheni bunduki,ambazo hutumika kushambulia raia wasio na hatia.

Chanzo - BBC Swahili

Zitto: Maisha yetu hatarini


Dodoma/Dar. Siku moja kabla ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni, ripoti ya uchunguzi wa IPTL kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe amesema amekuwa akipata vitisho ili kuzuia ripoti hiyo.

Akizungumza jana, Zitto alisema pamoja na vitisho hivyo haogopi kwa kuwa maisha yake ameshayaweka nadhiri siku nyingi.

“Kuna kundi la wahuni kutoka Musoma limeletwa Dodoma likiongozwa na mtu (jina tunalihifadhi) mwenye rekodi ya ujambazi. Hivi sasa anashikiliwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka zilizoibwa Ofisi ya Bunge. Usalama wa wajumbe wote wa PAC upo shakani,” alisema Zitto.

Aliongeza kuwa kuna vipeperushi vimesambazwa mjini Dodoma kumkashifu lakini havitamsumbua kwa kuwa yeye anataka ukweli ujulikane.

Baadhi ya wabunge jana walionekana na kitabu kilichoandikwa ‘mjue Zitto Kabwe kama mtetezi wa wanyonge,’ lakini ndani yake kikiwa na mambo ya kumchafua mbunge huyo.

Vitabu hivyo vinaelezwa kusambazwa kwa wabunge katika nyumba zao vikilenga kuonyesha kwamba Zitto hafai kusimamia PAC ambayo hivi sasa inashughulikia escrow.

Wakati Zitto akisema hayo, suala hilo la vitisho jana pia liliibuka bungeni baada ya Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed kueleza kuwa hali ni tete kuhusu usalama wa wabunge kutokana na escrow.

Akiuliza swali la nyongeza, Mohamed alisema usalama wa wabunge uko shakani kuanzia maeneo wanayofanyia kazi na makazi yao na hasa kipindi hiki tangu kuanza kwa sakata la escrow.

“Je, nini tamko la Serikali juu ya ulinzi na usalama wa wabunge katika maeneo ya kazi, pia katika maeneo yao ambayo wanaishi?” alihoji.

Kabla ya majibu kutolewa na Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye jana alianza kuongoza vikao baada ya safari yake nje ya nchi, aliingilia kati akisema ofisi yake inakusudia kujenga kijiji cha wabunge ambako watalindwa kwa pamoja.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba alisema Serikali inafanya tathmini ya vitisho vyote vya viongozi nchini wakiwamo wabunge ili kuhakikisha wanakuwa salama.

Nyaraka feki
Taarifa za kusambazwa kwa ripoti ‘feki’ ya IPTL jana ziliwagawa wabunge, baadhi wakitaka lijadiliwe huku Spika Makinda akipinga.

Tangu juzi, zimekuwapo taarifa za mtu mmoja kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka akidaiwa kuzisambaza zikiwa zimenyofolewa kurasa, zikidaiwa kuibwa katika Ofisi ya Bunge, lakini polisi walipomhoji alisema alipewa na mbunge mmoja.

Hoja ya kutaka suala hilo lijadiliwe ilitolewa na Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi akisema kuna umuhimu wa kujadili suala hilo na kutoa maagizo ya kina kwa Serikali.

“Inavyoonekana taarifa hiyo imeibwa baada ya kupokewa na Ofisi ya Bunge kwani katika ukurasa wake wa juu kuna muhuri wa Bunge na inaonekana imepokewa Novemba 14 na Ofisi ya Katibu wa Bunge,” alisema Mbatia.

Alisema kwa maelezo waliyopata ni kuwa taarifa inayosambazwa imeibwa kabla ya kuwasilishwa PAC iliyopewa jukumu la kuipitia na kupendekeza hatua za kuchukua.

“Baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa kwenye kamati hiyo, kuna alama iliyowekwa kwenye nakala zote na katika taarifa inayosambazwa alama hiyo haipo,” alisisitiza Mbatia.

Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 31 (g) cha Sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge, ni kosa kwa mtu yeyote kusambaza waraka wowote ulioandaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni kabla ya wakati wake.

Alisema adhabu ya kosa hilo ni faini ya Sh500,000 au kifungo cha miaka mitatu jela na kuwa kitendo hicho kinalenga kuliziba mdomo Bunge lisifanye kazi yake ipasavyo.

Baada ya kauli ya Mbatia, wabunge kadhaa walisimama kuonyesha kuiunga mkono, lakini Spika Makinda aliipinga.

Licha ya kumpongeza Mbatia na wenzake walioamua kufuatilia taarifa za kusambazwa na nyaraka hizo na kutoa taarifa, alisema anayehusika kuzisambaza ameshakamatwa na polisi, atashikiliwa mpaka atakaposema taarifa anazozisambaza amezitoa wapi.

“Ndiyo kazi inayoendelea sasa, wamefikia mahali (polisi) wanatumia ofisi yao kubwa ya Dar es Salaam kutambua mashine zilizochapa hizo taarifa ni za nani. Kifungu cha 31 cha Kanuni za Bunge kipo wazi, sasa tunajadili nini wakati mhusika yupo ndani?” alisema Makinda.

Kauli hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge kuanza kuzomea, lakini Spika Makinda alisisitiza kwamba suala hilo haliwezi kujadiliwa bungeni.

“Si kama natumia ubabe, nyaraka ilizopewa PAC zina alama maalumu na polisi wanafanya uchunguzi wa jambo hili. Hii ni nchi inaendeshwa kwa utaratibu si kwa kuzomeana.”

Kauli hiyo haikuwaridhisha wabunge na kwa mara ya pili walisimama na kuomba mwongozo na Spika Makinda alikubali miongozo iliyoombwa na viongozi tu wa kamati za Bunge na kambi ya upinzani bungeni.

Mbunge wa kwanza kupewa nafasi alikuwa Habib Mnyaa, Mkanyageni (CUF), ambaye aliomba suala hilo kujadiliwa kwa sababu Bunge halitajadili kesi inayomkabili anayetuhumiwa kusambaza taarifa.

“Hili suala linahusu Haki na Kinga ya Madaraka ya Bunge. Hali ya Dodoma imechafuka na kuna nyaraka zinasambazwa kwa wabunge majumbani mwao, hata wewe Spika (Makinda) unatajwa kuwa umechukua Dola milioni moja na unatafutiwa nyaraka usambazwe ili uchafuliwe,” alisema.

Akijibu suala hilo, Makinda alisema tatizo la wabunge ni kutaka kulipeleka suala hilo jinsi wanavyotaka wao, lakini kama na yeye ametafuna fedha yupo tayari kuonyeshwa hizo taarifa za kuhusika kwake.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye anakaimu nafasi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, akinukuu Kanuni ya Bunge ya 51 (3), alisema:

“Kanuni inasema likitajwa suala linalohusu haki za Bunge, Spika atampa nafasi mbunge husika kutoa hoja yake kisha hoja hiyo itapewa kipaumbele katika kupanga shughuli nyingine zote za kikao kinachohusika. Spika umekiri kuwa suala hili linahusu haki ya Bunge, vipi tusijadili?”

Licha ya hoja hiyo ya Lissu, Spika Makinda alisema kama suala hilo lingekuwa halijafika polisi lingeweza kujadiliwa, lakini kwa hali ilivyo sasa ni lazima polisi wamalize uchunguzi wao.

Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka naye aliomba mwongozo akitaka wabunge wapatiwe mapema ripoti ya PAC na CAG ili wazisome kabla ya kuanza kwa mjadala, ombi ambalo Spika Makinda alisema linafanyiwa kazi na Ofisi ya Bunge.

Awali, katika hoja yake Mbatia alisema Ijumaa iliyopita Ofisi ya Bunge ilipokea taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusiana na miamala inayofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa Kampuni ya IPTL.

Alisema Novemba 17, Naibu Spika, Job Ndugai alikabidhi taarifa hiyo katika Kamati ya PAC ili iichambue na baadaye kuwasilishwa bungeni.

Alisema walitoa taarifa kwa Katibu wa Bunge ambaye kwa kushirikiana na polisi walifanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na nakala nyingi za taarifa hiyo. 

Tucta: Washtakiwe
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, (Tucta) limeitaka Serikali kuhakikisha inawafikisha mahakamani viongozi wote watakaobainika kuchota fedha za escrow badala ya kuishia kujiuzulu.

Rais wa Tucta, Gratian Mukoba alisema imeshazoeleka kwa viongozi wa Serikali kujiuzulu pindi wanapobainika kuhusika na wizi wa mali au fedha za umma badala ya kufikishwa mahakamani.

“Tunaposema fedha za umma ni zile zinazotokana na wafanyakazi kukatwa mishahara yao kwa ajili ya kulipa kodi ijulikanayo kama “Lipa kadri unavyopata”, hii ndiyo kodi pekee ambayo haikwepeki na haiwezi kulipwa chini ya kiwango,” alisema. 

Imeandikwa na Fidelis Butahe na Hussein Issa (Dar), Sharon Sauwa na Boniface Meena (Dodoma).
Chanzo - Mwananchi

Pele back in hospital after Brazil legend treated in Sao Paulo for urinary infection

  • Pele admitted to the Albert Einstein Hospital in Sao Paulo on Monday
  • The 74-year-old had operation to remove kidney stones earlier this month
  • Three-time World Cup winner regarded as the one of the best players ever

Three-time World Cup winner Pele was taken to hospital on Monday with an urinary infection.

It was the second time this month he has been admitted for medical treatment.

The 74-year old was admitted to the Albert Einstein Hospital in Sao Paulo. A hospital spokesman said he had been admitted for a 'medical evaluation' and was in a 'stable' condition.

Pele was released from the same hospital less than 10 days ago after successfully undergoing surgery to remove kidney stones.

The Brazil legend won three World Cups as a player and was named 'Football Player of the Century' by FIFA, 'Athlete of the Century' by the International Olympic Committee, and a 'national treasure' by Brazil's government. 

Muhongo ahusishwa wizi nyaraka za Escrow bungeni


Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, ametajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mmoja kati ya vijana wawili wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi  mkoani hapa kwa tuhuma za kuiba kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge ripoti ya ukaguzi wa hesabu za zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa kifisadi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ukaguzi huo ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).Wakati Waziri Muhongo akitajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mtuhumiwa huyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye jana ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuongoza Bunge tangu lianze Novemba 4, mwaka huu, anadaiwa kutajwa kuwamo katika orodha ya vigogo waliovuna fedha hizo, huku yeye akipata mgawo wa Dola za Marekani milioni moja.

Aliyemtaja Waziri Muhongo kuwa na uhusiano wa karibu na kijana huyo, ni Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.

Mnyika alimtaja Waziri Muhongo, wakati akichangia mjadala kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2014, bungeni jana.

Muswada huo uliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni, Ijumaa wiki iliyopita.

”Mheshimiwa Spika, ni muhimu ofisi yako ifuatilie. Kwa sababu mtuhumiwa yule ana uhusiano wa karibu sana na Prof. Sospeter Muhongo, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa kwenye kashfa tunazozijadili,” alisema Mnyika.

Aliongeza: “Sasa nasema haya mapema ili isifikie hatua tukatumiwa kisingizio cha mambo kuwa mahakamani kushindwa kuwataja kwa majina wahusika. Polisi wafanye uchunguzi, wachukue hatua.”

Mnyika alisema uharamia kwenye suala IPTL wa muda mrefu umezidi mipaka.

Alisema taarifa alizonazo ni kwamba, polisi wanamshauri Spika wa Bunge kwa sababu wanataka haraka haraka wamkimbize mtuhumiwa huyo mahakamani ili baada ya hapo alieleze Bunge kuwa kishapelekwa mahakamani, hivyo hakuna sababu ya kutaja jina wala suala lake kujadiliwa.

Mnyika alisema tangu siku waliyowapa polisi taarifa, mpaka leo wamekuwa wakisitasita wakishindwa kutaja jina la mtuhumiwa, huku wakisingizia uchunguzi.
Hata hivyo, alisema upande wa serikali wanapokutana nao kwenye korido wamekuwa wakiwaambia kuwa mhusika anafahamika, ikiwa ni pamoja na watu wote ambao amekuwa akiwasiliana nao.

“Mheshimiwa Spika, ukiendelea kuyakinga mambo haya kwa kisingizio cha mambo kuwa polisi, halafu baadaye polisi wakaenda mahakamani, ukaja kuyakinga hapa kwa kisingizio cha kwamba mambo yako mahakamani, maana yake Mheshimiwa Spika na wewe utahesabika kwamba, hizo mbinu za hao maharamia waliopora ripoti ndani ya ofisi yako pengine na ofisi yako inahusika,” alisema Mnyika.

Alimshauri Spika Makinda kuwasiliana na vyombo vinavyohusika ili ofisi yake na kiti chake visitumiwe na watuhumiwa kuficha uharamia unaoendelea dhidi ya Bunge na uwajibikaji, ambao Bunge linapaswa kuusimamia kwa niaba ya wananchi.

Madai hayo ya Mnyika yalitolewa siku moja baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, kukaririwa akisema kuwa katika mahojiano na polisi, kijana huyo alikiri kwamba, alipewa ripoti hiyo na Mbunge mmoja, ambaye alikataa kutaja jina lake ili kuepusha kuharibu upelelezi.

Vijana hao walikamatwa na polisi Jumamosi wiki iliyopita, mjini hapa, baada ya kukutwa wakiwa na ripoti hiyo yenye mhuri wa Katibu wa Bunge, ambayo wanadaiwa ‘kuichakachua’ kabla ya kuidurufu na kuisambaza mitaani kama njugu.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, pia alithibitisha kutoa taarifa polisi kuhusu vijana hao kumiliki nyaraka zenye muhuri wa ofisi yake isivyo halali.
Kamanda Misime alisema hadi juzi vijana hao walikuwa wanashikiliwa na polisi.

SPIKA ATAJWA KUVUNA ESCROW
Madai juu ya Spika Makinda kutajwa kuwamo katika orodha ya vigogo waliofaidi mgawo wa fedha hizo, yalitolewa bungeni jana na Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Habib Mnyaa, kupitia mwongozo aliouomba chini ya kanuni ya Bunge ya 68 (7).

Mnyaa alisema madai hayo ni katika mlolongo wa hali ya hewa kuchafuka mkoani Dodoma tangu mjadala kuhusu kashfa hiyo upambe moto bungeni.
Alisema hayo alipokuwa akijaribu kumshinikiza Spika Makinda aruhusu Bunge lisimamishe shughuli zake zote za jana lijadili suala la ripoti hiyo kuibwa, kudurufiwa na kusambazwa mitaani.

”Kwamba hivi sasa hali ya Dodoma kwa ujumla Mheshimiwa Spika imechafuka. Imechafuka. Kuna nyaraka zinasambazwa, wanatiliwa wabunge nyumbani mwao wanapoishi ambazo zina kuchafuliwa wabunge,” alisema Mnyaa.

Aliongeza: “Mheshimiwa Spika, katika kuchafuliwa, wameshachafuliwa wengine hawa wajumbe wa PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali). Na hivi sasa minong’ono hata wewe unatamkwa kwamba umechukua dola milioni moja na unatafutiwa documents (nyaraka) kusambazwa na wewe uchafuliwe.”

Kutokana na hali hiyo, aliomba suala hilo lijadiliwe na Bunge kama, ambavyo Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, alivyoomba kupitia hoja aliyoitoa bungeni jana.
Alisema mjadala kuhusu suala hilo ni mpana na kwamba, hauhusiani na kesi ya kukamatwa kwa vijana hao, ambayo iko polisi.

“Mjadala unahusiana na zile tulizosema haki na kinga za madaraka ya Bunge. Hili suala tunahitaji kujadili si kwa suala la kesi iliyoko polisi, tuna suala la kujadili haki na madaraka ya Bunge na namna gani Bunge lako liamue kutumia kiti chako,” alisema Mnyaa.

Aliongeza: “Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima tunaomba uruhusu mjadala huu japo kwa nusu saa ili tulishauri Bunge na kiti chako tuweze kuamua. Naomba kuwasilisha.”

SPIKA MAKINDA AJIBU
Baada ya Mnyaa kueleza hayo, alisimama Spika Makinda na kusema kama kweli naye amechukua dola milioni moja, basi wabunge watalionyesha hilo bungeni .

”Mtanionyesha, mtanionyesha,” alisema Spika Makinda na kusababisha kuzua zogo bungeni jana.

Awali, wabunge jana waliwasha moto bungeni, huku wakibishana, wakishinikiza kiti cha Spika kupeleka mapema ripoti hiyo ya CAG ili wapate muda mpana wa kuijadili.

Wabunge hao walichafua hali ya hewa kwa mara nyingine tena baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, wakiunga mkono hoja ya Mbatia aliyetaka Bunge liahirishe shughuli zote zilizopangwa ili Spika awape wabunge muda wa kujadili hoja ya kusambazwa kwa ripoti hiyo ya CAG.

Mbatia aliomba mwongozo huo chini ya kifungu cha 51 cha kanuni za Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

“Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja ya kusitisha shughuli za kujadili suala linalohusu haki za Bunge lililotolewa katika kanuni ya 51 ya kanuni za Bunge toleo mwaka 2013,” alisema Mbatia.

Pamoja na mambo mengine, alisema inasadikiwa kuwa mtuhumiwa huyo anahusika katika kudurufu na kusambaza taarifa husika na mpaka sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi. Mbatia alisema inaonekana kuwa ripoti hiyo imeibiwa baada ya kupokelewa na Ofisi ya Spika, kwani katika ukurasa wa juu kabisa kuna muhuri unaosomeka ‘Ofisi ya Katibu wa Bunge’, imepokelewa Novemba 14, mwaka huu, sanduku la Posta 941 Dodoma.

Alisema kwa mujibu wa maelezo waliyopewa ni kuwa, inawezekana taarifa inayosambazwa imeibwa kabla ya kuwasilishwa kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwani baada ya kuwasilishwa kwenye kamati hiyo kuna alama maalumu, ambayo iliwekwa kwenye nakala zote, ambayo haipo katika taarifa hiyo inayosambazwa.

“Mheshimiwa Spika, kitendo cha taarifa hiyo kusambazwa mitaani wakati kamati ya PAC ikiwa inaendelea na uchambuzi wake kinamaanisha kuwa kuna watu wamejipanga kuchafua uongozi wa Bunge hili, kushusha hadhi ya Bunge, kuzuia Bunge lisifanye kazi yake kikamilifu,” alisema Mbatia.

Aliongeza: “Kifungu cha 31(G) cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge sura 296 kinaainisha kuwa ni kosa kwa mtu yeyote kusambaza nyaraka yoyote iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni kabla ya wakati wake.”

Alisema kumekuwa na jitihada nyingi za wazi wazi na za kificho zinazoonekana kulenga kuzuia Bunge lishindwe kufanya kazi yake katika suala hilo.

Mbatia alisema wizi huo na usambazaji wa taarifa ya ukaguzi maalumu kabla haijawasilishwa bungeni, ni vitendo vinavyotakiwa kukemewa na kutolewa tamko kali la Bunge.
“Kwa kutumia kanuni ya 51 ya kanuni za Bunge ya toleo la Bunge la mwaka 2015, naomba kutoa hoja sasa Bunge lako lisitishe shughuli zake zilizopangwa kufanyika hivi sasa ili wabunge wapate fursa ya kulijadili suala hili kwa kina na kutoa maagizo yanayostahili kwa serikali. Mheshimiwa Spika kwa unyenyekevu mkubwa naomba kutoa hoja,” alisema Mbatia.

Hoja hiyo ya Mbatia, iliungwa mkono na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye alisisitiza kutaka suala hilo lijadiliwe ili hali ya hewa iliyochafuka iondolewe.

Akijibu hoja hiyo baada ya wabunge kusimama kuiunga mkono, Makinda alisema hakubaliani nayo.“Hoja haikubaliki, hebu kaeni huko, huwa hakuna hoja ya aina hiyo. Kaeni, someni kifungu namba 51, naomba tusikilizane,” alisema Makinda.

Aliongeza: “kwanza kabisa mimi lazima nikiri kwamba namshukuru bwana Mbatia na wenzake kwa kazi waliyoifanya ya kuchunguza hiki wanachokisema, wamefanya kazi kubwa.” Alisema baada ya kufanya hivyo, aliyehusika amekamatwa na yuko ndani na kwamba, mpaka sasa Ofisi ya Bunge inashirikiana na polisi kutokumtoa huyo mtu mpaka aseme vitu alivyokuwa anavisambaza amevitoa wapi.

“Hiyo ndiyo kazi inayoendelea mpaka sasa hivi, wanafika mahali mpaka kutumia ofisi yao kubwa ya Dar es Saalam ili kutambulisha kwamba mashine zilizochapa zile ni za nani,” alisema Makinda.

Alisema kwa kutumia kifungu cha haki za wabunge na kinga namba 31, suala hilo linashughulikiwa na kwamba, mtuhumiwa huyo akithibitika alitenda ndiyo atahukumiwa kifungo cha miaka mitatu au faini inayohusika.

Kutokana na hali hiyo, alisema suala hilo haliwezi kujadiliwa wakati mtuhumiwa huyo akiwa bado yuko ndani.

“Waheshimiwa wabunge, naomba tuelewane sisi ni wabunge, mnajadili kitu gani? Huyo mtu amewekwa ndani ‘ndiyo’ waheshimiwa wabunge sikilizeni hatuendeshi Bunge kwa kupiga kelele tuelewane, nasema hili swali tunaliacha kwanza, nawaambia mi nitapanga muda, tukipata taarifa ya polisi,” alisema Makinda, huku akizongwa na makelele ya wabunge.

Akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM),  Spika Makinda alisema ofisi yake inalishughulikia kwa umakini mkubwa suala hilo na mara tu uchunguzi wa kamati na ule wa polisi utakapokamilika ripoti hiyo itapelekwa bungeni na wabunge watapata fursa ya kujadili na kufikia maamuzi.

“Wabunge msiwe na wasiwasi hili suala liko wazi na linakwenda kwa utaratibu hivyo vuteni subira tutalileta  humu ndani na litajadiliwa,” alisema Makinda.

Alisema ofisi yake imeshaweka utaratibu wa kuhakikisha ripoti ya CAG inawafikia wabunge mapema iwezekanavyo kabla ya kufikishwa kwa taarifa ya PAC bungeni.

Spika Makinda alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha wabunge kupata muda mzuri wa kuisoma ripoti hiyo na kuielewa vizuri kabla ya kuanza kuijadili Novemba 26, 27 na 28 itakapowasilishwa mbele ya Bunge.

Alisema ofisi yake imeiongezea nguvu PAC kwa wajumbe watatu, ambao ni Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), Mbunge Mwibara, Kangi Lugola (CCM) na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangwalla (CCM). Katika muongozo wake aliouomba chini ya kanuni ya 68 (7), Sendeka alitaka kujua ni kwanini Spika asimuelekeze Katibu wa Bunge kuhakikisha ripoti ya CAG inapatikana kwa wabunge jana badala ya kupatikana mitaani ili waisome pamoja na vielelezo vyake na kuitendea haki.

KAMANDA MISIME
Kamanda Misime alisema jana kuwa bado wanamshikilia mtu mmoja (hakutaja jina) anayehusishwa na usambazaji wa nyaraka hizo.

Alisema kwa sasa utambulisho wa mtu huyo unahifadhiwa, ili kulinda mazingira ya upelelezi wanaoufanya kuhusu tukio hilo, ambapo inadaiwa kuwa nyaraka hizo ziliibwa kwenye ofisi za viongozi wakuu wa Bunge.

“Kwa sasa tunachunguza mambo mengi nyeti, ikiwamo kubaini kama nyaraka hizi ni ripoti halisi za Takukuru na CAG, ikiwa muhuri uliyo kwenye nyaraka hizi ni wa Katibu wa Bunge na uhusiano uliyopo kati ya mmoja wa watuhumiwa wa Escrow na huyu jamaa,” alisema. Misime.

NA MUHIBU SAID
CHANZO: NIPASHE

Wavuvi 50 wauawa na Boko Haram


Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya shambulizi lengine kubwa sana na kuwaua takriban wafanya biashara 50 wa kuuza Samaki katika ufuo wa ziwa Chad.
Shambulio hilo lilifanyika Alhamisi lakini kutokana na matatizo ya kimitambo, taarifa za mauaji hayo hazikuweza kutolewa punde yalipofanyika.
Siku moja kabla ya mauaji hayo, zaidi ya watu arobaini waliuwa na wanamgambo hao, katika shambulizi lililofanya peupe mchana katika jimbo la Borno.
Wafanyabiashara hao, walikuwa njiani kununua Samaki waliposhambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Boko Haram waliziba barabara karibu na kijiji cha Doron Baga na kulingana na kiongozi mkuu wa shirika la wafanyakazi hao wakawachinja wengi wa waathiriwa wengine wakifungwa kamba na kuzamishwa majini katika ziwa Chad.
Nia ya shambulizi lao haikujulikana mara moja.
Eneo lililoshambuliwa linapaswa kuwa na kikosi cha wanajeshi kinachoshika doria, lakini kikosi cha wanajeshi hao kutoka Nigeria , Chad na Niger hakijaweza kudhibiti hali katika eneo lenyewe kama ilivyotarajiwa kwani wameshindwa kulikomesha kundi la Boko Haram kufanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Hili lilikuwa shambulizi la pili kubwa kufanyika katika jimbo la Borno wiki jana na kwa jumla takriban watu 100 waliuawa.
Mnamo siku ya Jumatano, wapiganaji hao walivamia soko moja katika eneo la Aazara Kuya. Watu 45 walikamatwa huku wakifungwa mikono na kukatwa koo zao.
Shambulizi hili inaarifiwa lililengwa kuadhibu jamii baada ya wanamgambo wanne kutambulishwa kwa wanajeshi na kuuawa.

Chanzo - BBC Swahili

 
Re - Design by ChingaOne | Blogger Theme by Lasantha - Free Blogger Themes | NewBloggerThemes.com